“Nikipiga Picha Za Utupu Nalipwa, Wazazi Waangalieni Watoto Wenu”- Huddah

Socialite maarufu kutoka Kenya mrembo Huddah Monroe maarufu kama Huddah The Boss Chick amewatolea povu wazazi wanaomsema kuwa kuanika picha zake za Utupu Mtandaoni zinaharibu watoto wao wa kike wanaomfuatilia.

Huddah amejizolea umaarufu zaidi kutokana na umbo lake matata Lakini pia anajulikana kwa kuanika umbo lake Kwenye mitandao ya kijamii huku akiwa mtupu kabisa au nusu utupu.

download latest music    

Kutokana na Kuposti picha hizo Huddah amekuwa akikosolewa sana kutokana yeye kuwa maarufu na kioo  cha jamii ametakiwa kuwa mfano mzuri kwa watoto wa kike wanaomfuatilia.

Lakini Huddah ameibuka na kujitetea kuwa anapoweka picha kama hizo Kwenye mitandao ya kijamii ni kwa sababu anakuwa analipwa kufanya hivyo aidha ni kwa ajili ya kutangaza nguo zile za ndani au kutangaza mahoteli ya kifahari.

Wasichana wengi wananiangalia mimi. Sidhani kama nimemshawishi mtu yoyote kupiga picha za utupu. Tatizo linakuwa lipo kwa wazazi wanaoshindwa kulea watoto wao na kijamii Kwenye mitandao ya kijamii kuangalia Huddah kufanya nini”.

Lakini pia Huddha aliendelea kusisitiza kuwa kuposti picha na nguo za ndani ni kazi yake inayomuingizia kipato:

Mara nyingi nikipiga picha na nguo za ndani nakuwa nafanya matangazo ya biashara aidha natangaza hoteli au nguo za ndani nilizovaa na nifanya hivyo kwa sababu nalipwa Sifanyi ovyo ovyo”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.