Nikitoa Ngoma Anakufa Mtu :Mboso

sanii kutoka kundi la wcb, Mboso amefunguka  na kuelezea kwa undani juu ya changamoto na mafanikio aliyoyapata kwa mwaka huu huku akisema kuwa  umekuwa mwaka wa neema kwa sababu ya nyimbo zake lakini upande mwingi kunakuwa na tatizo.

Mbosso amesema kuwa mwaka jana alikuwa na mkosi kwani kila alivyoachia video ya ngoma mpya, siku hiyo hiyo kulitokea msiba mkubwa Tanzania.

download latest music    

Kuna vitu vilikuwa vinatia unyonge. Mwaka 2018 kuna watu walikuwa hawajajua kwamba kila nikitoa wimbo, lazima utokee msiba. Kila nikitoa wimbo, kila nikiweka video. Nakumbuka kipindi natoa Nadekezwa kulitokea Msiba wa mtoto wa dada mmoja anaitwa Muna. Kipindi nakuja kutoa Nipepee kulitokea msiba wa mzee Majuto. Nilivyotoa Hodari kulitokea ajali ya MV Nyerere, nikawa nawaza kwanini zinatokea changamoto kama hizi? ilinipa stress sana.“ameeleza Mbosso kwenye mahojiano yake na Mseto East Africa.

Kwa upande mwingine, Mbosso amesema mwaka huu amejipanga kufanya kolabo na Sauti Sol na kuachia kolabo yake na Mr Flavour.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.