Nikki Wa Pili Alinifanya Niache Kurap – Dayna Nyange

Msanii wa muzuki wa Bongo Fleva  ambae kwa sasa anatamba na kibao chake cha Chovya mwanadada Dayna Nyange amefunguka na kusema kuwa kabla ajaanza  muziki alikuwa ni msanii wa kurap na alikuwa akimudu kufanya hivyo lakini alitokea mtu akamshauri kuachana na muziki huo kuwa haulipi ivyo afanye aina nyingine ya muziki.Mwanadada huyo anasema kuwa kwa kipindi cha mwanzoni alikuwa yupo vizuri katika kurap sana lakini alitokea Nikki wa Pili na kumwambia kuwa muziki wa aina iyo haulipi kabisa hivyo aachane nao.

“nakumbuka zamani nilikuwa nipo vizuri sana kwenye kurap  hadi nilitaka kusainiwa katika lebel ya Hermy B, B-hits kipindi icho tulikuwa tukifanya kazi pamoja na wakina AY , nakumbuka AY alikuwa akinisaidia hadi baadhi ya vitu vya kumuziki.Kipindi icho mtu kama AY ananisikiliza na kunionyesha nguvu yake katika muziki,najiona ukubwa wangu ulikuwa sehemu gani” anasema Dayna Nyange

download latest music    

Dayna anaendelea kusema kuwa lakini Nikki wa Pili ndio msanii aliemtoa katika kurap na kunipeleka katika kuimba, anasema ‘Nikki Wa Pili alimwambia atakuwa hapati ela endapo ataendelea kurap”Nikki wa Pili ndiye alinitoaa katika kurap na kunileta katika kuimba, aliniambia Dayna acha kurap utakuwa haupati ela aisee,, basi Nikki nakushuru,nikaaacha  na kurap kabisa na  nikaanza kuwa mwimbaji ” anafunguka Dayna

Dayna anaendlea kusema kuwa anashukuru kwa ushauri alioupata kutoka kwa Nikki kwa sababu umempa mafanikio makubwa sana, kwa sasa anatuzo kutokana na muziki huohuo”sasa hivi nina tuzo za BAE,AFRIMMA, so ninachoamini kila jambo lina wakati wake” aliongezea Dayna.

Mwanadada huyo ambae anafanya vizuri sana katika muziki amekuwa akitoa nyimbo nzuri pia , baadhi ya vibao vyake ni pamoja na ‘komela’ aliomshiriksha Billnass, ‘angejua’, ‘I do’, ‘Nivute kwako’ alioimba na Barnaba , ‘mimi na wewe’ na huu mpya unaojulikana kama ‘chovya’.

Dayna Nyange pia ni mama wa mtoto mmoja wa kike na amekuwa mama bora kimalezii, lakini pia Dayna ni mmoja kati ya wasanii wa kike wasiokuwa na scandal katika mitandao

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.