Niko Busy Na Biashara- Harmorapa

Msanii wa muziki wa bongo fleva, aliyejulikana na kuwa maarufu kwenye game kutokana na drama zisizoisha , ameibuka na kusema kuwa wale wanaotangaza kuwa amefulia ni uongo ila yuko busy anafanya biashara zake.Harmorapa anasema kuwa ukiachana na maisha ya muziki , kuna kitu kingine anafanya tofauti na icho hivyo kwa muda huu mambo ya biashara yamemfanya kuwa busy ila anakaribia kurudi hivi karibuni na mashabiki wakae mkao wa kula.

Akiongea na eNews ya EATV, Harmorapa amesema kuwa watu inabidi wajue kuwa kuna maisha nje ya muziki,”watu waelewe  kuwa sipo kimya kuwa nimefulia, sasa hivi niko busy na biashara na pia nina safiri sana,ile kuonana tu ni bahati.Project zangu zinaendelea kama kawaida, na wiki ijayo naachia dude jipya, watu wajue mimi nipo ,tatizo wamezoea kuwa harmorapa kafanya hivi mara kafanya vile, kwa sasa niko busy na biashara na muziki wangu bado upo sana.kama kutrend kila siku na-trend, kila siku naingia instagram,nakuta tu mtu amenipost kwaiyo nakuwa najua kumbe bado nipo machoni pa watu.Bado mimi nipo  na muziki upo na vitu vitaendelea”

download latest music    

Kwa muda sasa Harmorapa amekuwa kuwa kimya , tofauti na jinsi alivyokuwa akichukua vichwa vya habari katika vyombo vya habari , na kuna baadhi ya watu wakaanza kusema kuwa inawezekana atakuwa amefulia, hivyo harmorapa kaamua kuwajibu wanaomzushia habari hizo na kwamba hivi karibuni anatoa wimbo mpya hivi wasubiri kitu kipya.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.