Nilishapata Proposal za Kwenda kwa Waganga Nyingi :-Kareen

Mwanadada Kareen lil ambae sasa hivi anatamba na wimbo wa lawana kutoka THT amefunguka na kusema kuwa amekuwa akipokea proposal nyingi kutoka kwa watu wakimwambia kuwa ili muziki wake ufanye vizuri basi aende kwa waganga wa kienyeji kuloga ili kuwa na nyota.

Kareen anasema kuwa hata hivyo hawezi kufanya kitu kama hicho kwa sababu familia yake haijamkuza katika malezi hayo ukizingatia kwao wanamfuata sana Mungu na wanasali sana hivyo sala za babu na bibi zake kwake ni baraka tosha.

download latest music    

Akiongezea kuhusu mziki wake Kareen anasema kuwa amekuwa akivutiwa sana na mwana dada vannesa kutokana na kuwa mni mwanamkziki wa kike anaefanya kazi na kufika mbali kwa nguvu zake mwenyewe .

Kareen ambae ni mtoto wa mtangazaji maarufu wa radio Gadner G Habash anasema kuwa kwa kiasi flani pia jinala baba yake limekuwa likisaidia ku-push mziki wake na amekuwa akipata shavu lakini pia muziki wake mzuri umemfikisha alipo.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.