NImeoa kwa Siri ” Beka Flavour

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Beka Flavour, ameweka wazi kuwa sasa yeye sio msela tena kwani amemuoa rasmi mama mtoto wake, anayejulikana kwa jina la Happy.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Beka Flavour amesea kwamba msichana huyo ambaye amezaa naye, ni mke wake rasmi kwani amemuoa kwa imani yake ya dini ya Kiislam, lakini hakutaka kuweka wazi kwa watu.

download latest music    

Mimi nimeoa kabisaa, japokuwa sio kila mtu anajua kuwa nimeoa, unajua ili mtu mwengine ajue kuwa umepitia taratibu zote na kihalali kabisa, lazima uweke wazi kwenye simu, mimi nimeoa kihalalai, si unajua sisi Waislamu mambo yetu chini chini, ila sijataka kuweka wazi”, 

Beka Flavour nameendelea kusema kwamba mke wake alilazimika kubadili dini ili waweze kufunga ndoa ya Kiislam, kwani awali alikuwa na imani ya Kikristu.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.