Nimependa na Kukubaliana na Uchaguzi wa Jokate- Irene Uwoya

Msanii katika tasnia ya Bongo Movie Irene Uwoya amefunguka na kuweka wazi kuwa amependa na amekubali kabisa katika uteuzi wa Msanii mwenzake Jokate Mwegelo ambaye ni Mkuu wa wilaya.

Uwoya amefunguka hayo wakati alipokuwa anajibu barua ya wazi ya msanii Rado ambaye alimhoji kuhusu ushiriki wake katika siasa na kudai anaona kama Uwoya amestahili pia kuchaguliwa kuwa mbunge.

download latest music    

Kama utakumbuka mwaka 2015, Irene Uwoya aligombania nafasi ya Ubunge viti maalumu CCM na kusema ukweli alifanya vyema sana lakini Rado amemuuliza Uwoya kama anataka kuenda mbele kama Jokate je Dogo Janja anafaa kuwa kama mume wake?

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Uwoya ametoa majibu kuhusu hilo ambapo ameweka wazi kuwa hana wivu wala tatizo na Jokate kuchaguliwa kwani anaheshimu maamuzi ya Raisi Magufuli.

Naamini sana katika maamuzi na mapendekezo ya mwenyekiti wangu wa Chama. Naamini sana na nimependa uteuzi wa Jokate kwa sababu baada ya kampeni na uchaguzi kuisha watu wengi tuliendelea na mambo yetu binafsi lakini ukifuatilia kwa ukaribu Jokate amepambana na amekuwa karibu sana na harakati za chama na haswa kushiriki katika shughuli za kijamii kwa haya na mengi zaidi nampongeza zaidi kwani amepanda mbegu nzuri ambayo amevuna mavuno mazuri hongera kwake Mheshimiwa Jokate Mwegelo”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.