Nimeshaumizwa Sana na Mapenzi Kwa Sasa Nipo Single-Aslay

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Aslay Isihaka amefunguka na kudai kuwa kutokana na kuumizwa sana na mapenzi kipindi cha nyuma amechukua maamuzi ya kuwa Single kwa sasa.

Hitmaker huyo wa goma la ‘Natamba’ ameweka wazi kuwa hataki kukurupuka na kuingia Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi kutokana na matukio aliyopitia kipindi cha nyuma.

download latest music    

Kwenye Interview aliyofanya na kipindi cha Leo ten cha Clouds Fm, Aslay ambaye amezaa mtoto mmoja na mama watoto anayejulikana kama Tessy Chocolate, ametiririka haya.

Nilishawahi kuumia kwenye mahusiano ya kimapenzi lakini mahusiano hayo hayakuwa kati yangu na mama mtoto wangu Tessy ni ya mwanamke mwingine, ndio maana kwa sasa nipo single“.

Sitaki kukurupuka kutafuta mahusino mapya kwa sababu wanawake wengine wanakupenda kwa kuwa ni msanii na wengine wana tamaa”.

Hivi sasa Aslay anafanya vyema na ngoma yake ya Kwatu ambayo inaendelea kufanya vyema Kwenye Media mbali mbali.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.