NInastahili Kuwa Msanii Wa WCB- Mbosso

Mwanamuziki wa Bongo fleva Marombosso maarufu kama Mbosso ambaye amesainiwa chini ya label ya WCB amefunguka na kusema kuna muda utafika watu wote watajua kuwa anastahili kuwa msanii wa WCB.

Mbosso amefunguka hayo baada ya kuona kuwa anakosolewa sana na baadhi ya watu ambao wanaona kama hana kipaji kikubwa cha kuweza kuwa msanii wa label hiyo.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na TBC Fm, Mbosso amefunguka na kuongea mengi kuhusiana na uwezo wake katika label hiyo:

Kuna muda unaweza ukafanya kitu kwako wewe kipo sawa na unajaribu kukiwakilisha kwa njia iliyo sawa lakini inafikia hatua anaona hakiko sawa anafikia hatua hata ya kukutukana matusi, inafikia hatua mtu anakutukana mpaka matusi ya mama yako.

Lakini huwezi kumzuia mtu kufanya hivyo vitu ila kuna muda utafiki kila mtu atajua Mbosso kumbe anastahili kuwa WCB au anastahili kupewa hiki ambacho anapewa sasa hivi“.

Mbosso alijipatia umaarufu wakati alipokuwa katika kundi la Yamoto Band, Baada ya kundi hilo kuvunjika Mbosso alijiunga na timu nzima ya WCB rasmi mwaka huu tarehe 28 januari.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.