Ninaweza Kumtuliza Chid Benz, Njia Rahisi ni Kumfunga :-T.I.D

Mwanamuziki wa siku nyingi T.I.D amefunguka alikuwa akiongea na radio station moja na kusema kuwa anasikitika sana anapomuona Chid Benz anashindwa kujiondoa katika madawa ya kulevya pamoja na jitihada zote ambazo ziliweka na wazazi pamoja na serikali kutaka  kumsaidia lakini bado anandelea.

Akiongea ka kujiamini kabisa, msanii huyo anasema kuwa ni vigumu sana kwa Chid Benz kutoka katika madawa ya kulevya kama atakuwa yuko uraiani na mweny uhuru, njia rahisi ni kumfungia ndani na kum-control kwa muda hata wa miezi sita akitoka huko atakuwa sawa.

download latest music    

T.I.D anasema kuwa kinachomuumiza ni kwamba hata unapompa salamu Chid Benz hakuna anachowaza zaidi ya kuomba pesa tu , na hicho sio kitu kizuri kwa msanii.

tunahitaji kumtuliza yule , hatuwezi kum-control kama atakuwa nje ya boundaries lazima ataenda tu atanunua atafanya nini, lakini tukimtuliza yule serious case six month ananyooka.Mimi naweza kumnyoosha lakini siwezi kwa sababu sijapewa majukumu hayo, lakini nikipewa nuvu nitamnyoosha , kwa sababu mimi nimeweza nitawashindwaje vijana wengine.

T.I.D aliwahi kujihusisha na madawa ya kulevya lakini alikuja kujitambua na kuomba msahana kwa mh paul makonda na ndipo aliposaidiwa na kutoka katika matumizi ya madawa ya kulevya.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.