Nini Akanusha Kuachana na Nay Kisa Wazazi.

Mwanadada mabe ni msanii wa bongo fleva nchini Nini amefunguka na kusema kuwa hakuna sababu ya wazazi iliyomsababisha yeye kuachana na mpenzi wake ambae pia alikuwa akifanya nae kazi Nay wa mitego.

Akiongea na Soudy Brown , nini anasema kuwa pamoja na kwamba Nay alisema kuwa wazazi wake ndio chanzo kikubwa vha yeye kuachana na mwanaume huyo lakini sio kweli kwa sababu wazazi wake hawajawahi kuingilia kabisa mahusinao yao .

download latest music    

Hata hivyo baada ya nini kuulizwa sababu kubwa ya kuachana na Nay , alisema kuwa alichoshwa na  vituko vya mwanaume huyo ukizingatia kuwa alikuwa akimfanyia vitu vya kinyama na kutembea na wanawake wengine huku wengne akiwaleta ndani na yeye mwenyewe akiwepo hivyo alivumilia kwa muda mrefu na sasa amechoka na kuamua kuachana nae.

Nini pia amekanusha tetesi zilizokuwa zikisambaa kuwa alikuwa akikaa na Nay nyumba moja hivyo walivyogombana na Nay kwa sasa amerudi nyumbani kwao kwamba sio kweli kuhusu hilo.

Mahusiano na Nay na Nini yalikuwa ya chii chini huku kila anayeulizwa anashindwa kukubali kuwa wapo katika mahusiano lakini cha kushangaza wamegombana kila mmoja amejikuta anatangaza katika ktandao ya kijamii.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.