Nisha Adai Anataka Mahusiano na Mwanaume Mwenye Pesa Kuliko Yeye

Muigizaji wa Bongo movie Salma Rajabu Nisha maarufu kama Nisha Bebe ameibuka na kuweka wazi hawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi ambaye amemzidi uwezo kipesa zaidi.

Nisha amefunguka kuwa inakuwa ngumu kwake kutembea na mwanaume ambaye hana pesa kwa sababu wengi wao aliokuwa nao na wakawa hawana kitu walikosa shukrani.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha Bongo 5, amedai wanaume wengi waliopita kwake walikuwa wanampenda kwaajili ya pesa lakini sio mapenzi ya kweli.

Nimeshadate tayari na watu ambao hawana mtonyo lakini mwisho wa siku hawana shukrani,” Nisha aliimbia Bongo5. “So kwa sasa hivi siwezi kudate na mtu ambaye nimempita kipato, lazima awe amenipita.

Wanaume wengi ambao walikuwa wanakuja kwangu walikuwa wanataka mpaka kununuliwa nguo, kila wiki wanataka shopping ya nguo, baby sijui nimeona kitu fulani kizuri, sijui nataka kile halafu mwisho wa siku hawana mapenzi wa kweli”.

Wiki iliyopita Nisha alianika Mahusiano Yake na Mzungu ambaye alikiri anajiweza na kipato cha kutosha na hivyo y hatahitaji kumlea.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.