Nisha Amfanyia MwanayeBonge La Party Nchini China

Muigizaji wa Bongo movie na Msanii wa Bongo fleva Salma Jabu maarufu Kama Nisha amekiri kumfanyia bonge la party nchini China binti yake mwenye umri a miaka 14.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Nisha amekiri kumfanyia party hiyo binti yake  huyo anayeitwa Ipsum kwa sababu ndiye kila kitu kwake kwani anaye huyo pekee hivyo anamfanyia kile kitu kinachomfurahisha maishani mwake ili afurahie uwepo wake.

Mwanangu nimemfanyia sherehe ya bethidei China ambayo imegharimu milioni nane, tumekuja kufanya huku maana ndipo alipopachagua nami kwa kuwa nampenda na ndiye mwanangu wa pekee nikamleta na amefurahi sana na anajivunia kuwa na mama kama mimi pia nafurahi kuwa na mtoto mkubwa hivi kwa sasa“.

Mastaa wengi wameonekana kwenda nje ya nchi na watoto wao na kufanya mambo ya kufuru ambapo Wiki chache zilizopita Aunty Ezekiel na yeye alimbeba binti yake Cookie na kwenda kufanya naye bonge la party nchini Dubai.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.