Nisha Aongea Na Wanaomkashifu Lulu Michael

Msanii wa bongo movies Salma Jabu maarufu kama Nisha  bebe, amefunguka na kuwaonya baadhi ya watu ambao tangu kesi ya msanii lulu michael ianze kusomwa katika mahakama jijini Dar Es Sallam wamekuwa mstari wa mbele kumuongelea mwanadada huyo.Msanii huyo amesema kuwa kwa kipindi kama hichi ambacho Lulu anapitia wakati mgumu sio muda wa kumnanga bali ni muda wa kumpa faraja na kumuombea apite katika kipindi ichi kigumu.

“tangu kesi ya Lulu ianze kusikilizwa upya, kuna watu wamekuwa wakimkashifu kila kukicha, kwa maneno ya ajabu bila kujua kuwa  hakuna ajuaye kesho yake, ni vyema tukampa faraja rafiki yetu, katika kipindi ichi kigumu anachokipitia” alifunguka Nisha

download latest music    

kwa kipindi cha muda mfupi ambacho Lulu amekipitia , akiwa anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia kumekuwa na maneno mengi katika mitandao yanayomsema vibaya mwanadada huyo,inawezekana kwa kukusudia au bila kukusudia lakini iki ni kipindi ambacho  mashabiki na watu wa karibu na Lulu wanapaswa kuwa na maneno ya kumpa  faraja ili aweze kushinda kesi hiyo, maamuzi mengine  na hukumu hutolewa na mahakama hivo watu wa mitandaoni hawapaswi kumuhuku msanii huyo.

Hata hivyo,imekuwa ni kama desturi kwa baadhi ya watu ambao wanakuwa haweleweki wamelalia upande gani, wanapoona mtu amefanya vizuri hujitokeza kumpongeza na anapopata matatizo wanaanza kumsema vibaya, huu ndio wakati ambao Lulu anapaswa kuiona nguvu kubwa ya mashabiki wake.

Kesi ya Lulu ambayo ilianza kusikilizwa Oktoba 19 , imeendelea jana ambapo Lulu alipata nafasi ya kuongea na kujitetea kwa nafasi yake,huku mashahidi wengine wakiwa tayari wameshatoa ushahidi wao kuhusu kifo cha marehemu kanumaba ambae alikuwa mpenzi wake na Lulu.Kifo icho kilitokea baada ya msanii huyo wa kike na mpenzi wake kuwa katika ugomvi uliosababisha purukushani za Kanumba kudondoka na kufa papo hapo.

Wapo baadhi ya watu maarufu na wasanii walionyesha kuwa karibu na Lulu Michael katika kipindi hiki kigumu kwa kutokea mahakamani na kumpa maneno yenye faraja mwanadada huyo akiwepo Dr.Cheni, na Muna love ambao muda wote wamekuwa nae mahakamani.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.