Nisha- Najutia Kuwa Kwenye Mahusiano Ya Kimapenzi na Viben 10

Muigizaji wa Bongo movie ambaye hivi karibuni amegeukia tasnia ya Bongo fleva, Nisha Bebe amefunguka na kukiri kuwa alishawahi kuwa na kiben 10.

Siku ya jana kuna video ilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii iliyomuonyesha Nisha akiwa anahesabu pesa huku akisema kuwa tangu ameacha tabia ya kulea viben10 amekuwa na pesa nyingi.

download latest music    

Nisha amekiri kuwa alishawahi kuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na kijana ambaye alikuwa amemzidi umri lakini amesema mara ya kwanza alipoanza naye Mahusiano hakujua hilo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo Tv, Nisha amefunguka haya kuhusu ishu hiyo:

Nimeshawahi kuwa Kwenye Mahusiano na mwanaume ambaye nimemzidi umri na ikitokea kwamba tulivyokutana sikufahamu kwamba nimemzidi umri lakini baada ya kuwa pamoja na kujuana zaidi ndio nikajua nimempita miaka kadhaa.

Lakini pia nimeshawahi kujutia kuwa na mwanaume ambaye nimemzidi umri   kwa  sababu mimi ndio nilikuwa kama namuhudumia kwa kila kitu na zaidi nilipoteza tu muda na nimejutia sana sana sana “.

Nisha ameweka wazi kuwa hivi sasa yupo Kwenye Mahusiano na mwanaume wa maana ambaye amemzidi kiumri na wanasaidiana katika mambo mbali mbali.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.