Nisha- Sijawahi Kuvaa Kigodoro Hili Umbo Nimepewa na Mungu

Muigizaji wa Bongo Movie Salma Jabu maarufu kama Nisha amefunguka na kudai umbo lake watu wanaloliona Kwenye picha ndio halisi na wala hajawahi kuvaa vigodoro.

Siku chache zilizopita Nisha alipata skendo ya kuvaa vigodoro vya kumuongezea shepu baada ya picha aliyoweka Mtandaoni kumuonyesha akiwa na maumbile makubwa tofauti na uhalisia wake.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Nisha amefunguka kuwa alichukua futi na kujipima makalio na matiti yake na kuwaangalia mastaa wanawake wenzake ambapo aligundua kwamba anawazidi sana na anamshukuru Mungu kwa kumpa zawadi hizo nzuri za kudumu.

Najikubali mwenyewe hata kama watu wakinishambulia, sijavaa kigodoro kwenye picha niliyoweka mtandaoni bali ni jinsi Mungu alivyonijaalia na hakuna staa wa kike anayenifikia, najivunia sana kwa kweli“.

Nisha ameshawahi kumwaga povu siku za nyuma baada ya mashabiki zake kumsema kuhusu kukosa shepu ambapo alidai aliyonayo imemtosha kabisa hivyo hahitaji mchina.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.