Nisha- Snura Hawezi Kuninyang’anya Bwana

Muigizaji wa Bongo movie Nisha amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusiana na habari zinazozagaa mtandaoni kuwa msanii wa Bongo fleva na aliyekuwa rafiki yake Snura Mushi amemuibia bwana ake.

Habari za Nisha kunyakuliwa bwana na rafiki yake Snurah zilisambaa wiki iliyopita baada ya Snurah kuweka wazi uhusiano wake na kijana anayeitwa Minu Calypto ambaye mwanzoni alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Nisha lakini baadae alionekana na Snurah.

download latest music    

Baada ya haari hizo kusambaa sana kwa kasi ya 4g Nisha mwenyewe ameamua kufunguka na kusema habari hizo hazina ukweli hata kidogo na kusisitiza kuwa hajachukuliwa bwana na mtu yeyote na hajawahi kugombea bwana na mtu.

Nisha amefunguka na kuiambia Enews ya East Africa TV kuwa habari hizo za yeye kuchukuliwa bwana na Snurah hazina ukweli wowote kwani yeye na mwanaume huyo waliachana miezi sita iliyopita na hata namba ya Simu ya Snurah yeye ndio aliyempatia.

Kwanza mimi sio mtu Wa kusimulia kila kitu ambacho ninacho huyo mkaka nilishaachana miezi sita sahivi Niko kwenye mahusiano mapya na mtu mwingine ambaye anajitambua, Snurah siwezi kumzungumzia sana kwasababu watu wanasema ameninichulia bwana na mimi nasema hajaninyang’anya bwana, kuninyang’anya ingekuwa kama bado Niko kwenye mahusiano na huyo mtu lakini tulishaachana”.

Lakini pia Nisha amesisitiza kuwa yeye na Snurah hawana bifu na pia bado ni marafiki wazuri tu bado wanaongea kwenye Simu kama kawaida na hata alivyomuomba namba ya yule mkaka hakuona soo kumpa kwa sababu walikuwa wameshaachana na yeye ameendelea na maisha mapya kwaiyo hakuna bifu kati yake na Snurah wala na Minu.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.