“Nishajikubali hali yangu” Wema Sepetu aongelea hali yake ya kushindwa kupata mtoto

Wema Sepetu amepoteza ujauzito zaidi ya mara mbili; mara ya mwisho mrembo huyo kuwa na mimba alikuwa anatajaria kupata watoto mapacha.

Ujauzito wa Wema Sepetu hata hivyo ulipotea ghafla Februari 2016, alikuwa na mahusiano na mchekeshaji Idris Sultan wakati huo.

download latest music    

Soma pia: Idris aongelea uchungu wa mama kupoteza ujauzito mwaka moja baada ya Wema Sepetu kupoteza mapacha wao

Wema Sepetu alilazimishwa kuongelea hali yake ya kushindwa kupata mtoto baada ya kupigwa vita kwenye mtandao wa Istagram.

Muigizaji huyo wa Bongo Movies aliwakashifu kina dada wajawazito kwa kuonyesha picha za nusu utupu. Wema alimsifu muigizaji mwenzake Esha Buheti kwa kusitiri ujauzito wake.

“Mashallah Esha wangu… Staha hadi Raha…. Sijawahi Elewa Wanawake wakishaenda kwenye Maternity shoots kwanini wanataka sana wakae uchi…. This Is Very Beautiful my Darling…. Allah Bariq Tumbo lako ujifungue salama my love… Unajua navyokupenda…. Hii iende kwa wanaokaaga Uchi wakiwa wanapiga picha za Mimba Jamani… ??? @esha.s.buheti,” aliandika Wema.

Esha Buheti

Watu wengine walimshambulia Wema kwa kudai kuwa mrembo huyo alikua anawaonea wivu kina dada wajawazito kwasababu yeye alishindwa kupata mtoto.

“Yaani ni Hivi, Hakunaga Jipya Now Mwaweza nitukana nikashtuka… Maana mi mwenyewe nishajikubali hali yangu… Labda niulize tu, Niko peke yangu nilokosa mtoto au ambaye sijazaa…??? HAPANA…!! Soooooooo Back to The Main Point, Nilichosema na nitakachoendelea Kusema, MUACHE KUTUWEKEA MIPICHA YA MITUMBO YENU YENYE MSTARI WA UJAUZITO… Yaani inshort, Muache kupiga picha za UTUPU kwenye Maternity Shoot zenu…. @esha.s.buheti Nakupenda mama…. You are the Definition of Womanhood & Motherhood… Na unajua Utamaduni wetu nini unataka…. Haya Wazungu endeleeni na Uzungu wenu…. Tukaneni na hapa pia…. Eti u thought I would keep quite jus cause mmeniita Jina nilolizoea… So nisi speak my Heart… Y’all are Very Funny….!!!! ??? Allah akutangulie kipenzi changu…. Baby,” Wema aliwajibu walompiga vita.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere