Nisher Aweka Wazi ukimya Wake Ulisababishwa na Msiba

Mtayarishaji wa nyimbo bongo,Nisher amefunguka kuwa kukaa kwake kimya wa muda mrefu kulisababishwa na matatizo tya kifamilia aliyokuwa ameyapata hasa kubwa la kufiwa na mtu wa karibu kabisa katika familia yake ambae ni babu yake.

Nisher ameweka wazi kuwa msiba huo ulimuathiri sana hivyo kufanya  ashindwe kufanya mambo mengi ikiwa pamoja na kukaa mbali na mashabiki na kazi zake.

download latest music    

siku 14 zilizopita zilikuwa siku ngumu sana kwangu lakini napedna kuchukua nafasi hii kuwaomba radhi  mashabiki wangu  na wadau wote mnaonisapoti kuwa  nilishindwa kabisa kupost au kuwa karibu na simu yangu kutokana na msiba wa babu yangu ulinilazimu kuacha kila kitu nilichokuwa nikikifanya dar na kwenda arusha kwa sababu mimi ndio mtoto wa kwanza katika familia yetu kuwa karibu na baba yabgu mabe siku ya birthday yake ilikuwa nsiku chache kabla ya kifo cha baba yake. hii imenigusa sana mimi pamoja na familia yetu na hii imetufanya tukutane na tuwe karibu kama familia  katika kipindi hiki kigumu .ijapokuwa babu alifariki katika umri mkubwa lakini bado tunakumbuka busara  na maneno yake ya hekima  najinsi alivyokuwa akipenda kila mtu awe na umoja na ushirikiano.naomba radhi kwa mashabiki na wadau wote kwa delay yoyote.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.