“Nitamlea Mwanangu Katika Misingi Ya Dini”-Jike Shupa

Video Queen aliyejizolea umaarufu Baada ya kuonekana kwenye video ya wimbo wa Nuh Mziwanda ‘Jike Shupa’ Zena Abdullah maarufu kama Jike Shupa amefunguka kuhusu ujauzito Wake.

Jike Shupa amesema kuwa akiwa katika miezi michache kukaribia kujifungua mtoto wake ameweka wazi kuwa anampango wa kumlea Mtoto Wake katika misingi ya kidini.

download latest music    

Wakati mwingine mipango kabla ya tukio ‘inamata’, maana Jike Shupa amejiapiza hivyo miezi minne kabla ya kujifungua kwake, ambapo amesema, akizubaa katika malezi mwanaye ajaye anaweza kufuata mkumbo wa maisha mabaya.

Natarajia kujifungua mwezi wa nne Mungu akipenda, sijaenda kupima ili nijue nitajifungua mtoto wa jinsia gani, lakini natarajia siku za hivi karibuni nifanye hivyo kwa kuwa natamani nijue nimebeba kiumbe cha jinsia gani“.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.