Noti ya Elfu Kumi Yamtesa Soudy Brown .

Moja ya viongozi wa kituo cha polisi amethibitisha taarifa kuwa msanii Maua Sama pamoja na mtangazaji wa Clouds Media Soudy brown wamekamatwa na polisi siku ya jana wakituhumiwa kwa kosa la kuidharirisha pesa ya serikali.

Mtu wa kwanza kutoa taarifa hiyo alikuwa ni mtayarishaji wa muziki Abbah ambae alisema kuwa  Maua Sama pamoja na Soudy brown walikuwa wote ndani lakini baadae yeye alitolewa na kuwaacha wenzake ndani.

download latest music    

Hata hivyo baada ya  hapo  kiongozi wa kituo cha polisi walichokamatwa  wasanii hao alithibitisha swala hilo  na kusema kuwa “ni kweli hawa watu tunao na tumewaweka ndani, mwingine jana na mwingine leo lakini kwa sasa  tumewashikilia watu hawa na tunatafuta wapelelezi wa kesi hiyo .

Hata hivyo polisi huyo anasema kuwa  kosa kubwa walilofanya watu  hawa ni kudharirisha pesa ya serikali  kutokana na video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha maua sama akiwa anakanyaga pesa ya noti ya shilingi elfu 10.

 

 

 

 

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.