Nuh Mziwanda akiri kubadili dini

Mkali wa Bongo Fleva Nuh Mziwanda amesema kuwa Sasa yeye ameirudia dini yake ya kwanza, Mkristo, baada kuachana na aliyekuwa mke wake.

Nuh alisema haya baada ya kuzungumza na XXL ya Clouds FM, huku aliendelea kusema ni kweli alikuwa kanisani Jumapili hii iliyopita na kukiri kuwa habari zinazoenea mitandaoni ni za kweli. Msanii huyu alisema;

download latest music    

“Nimerudi kwa Mungu wangu ili mambo yangu yaende vizuri maana tunafanya muziki wa dunia anatusamehe ila kurudi kwake pia ni jambo la kawaida sana.”

Aliendelea kwa kujibu tariffs zilizotolewa na aliyekuwa mke wake kuwa ameacha kumjali mtoto wake. Nuh alisema;

“Mara ya mwisho nilikuwa na Anyagile kwenye photoshoot ya ngoma yangu mpya jana kwa Mx Carter, inayotoka hivi karibuni sasa yeye anavyosema sijamuona mtoto muda mrefu sijui anamaanisha nini. Anaongea vibaya kwenye media sio vizuri, mimi na fan base yeye mwanamke anatakiwa ajue anaongea nini, ila muache aongee akikua ataacha, vile vile mimi sina tatizo naye kama kaolewa, yeye si ndio kaamau mimi bado kijana na kila mtu anafanya anachotaka mimi nimemrudia mungu huwezi jua atanipatia mke mwingine mwema”.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua