Nuh Mziwanda Amtaka Diamond Aache Kudhalilisha Wanawake

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nuh Mziwanda amemjia juu msanii mwenzake Diamond Platnumz na kumtaka aache vitendo vyake anavyofanya vinavyopelekea kudhalilisha wanawake.

Nih ameongelea kitendo cha Diamond kusabaza video Kwenye mitandao ya kijamii akiwa na wanawake wawili tofauti katika usiku mmoja kama udhalilishaji wa wanawake.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Nuh Mziwanda amedai kitendo alichokifanya Diamond sio cha kiungwana kwani wanawake wote ni kama mama zetu hivyo tunapaswa kuwaheshimu.

Ni lazima tuwaheshimu wanawake maana ndio waliotuzaa na waliotuleta duniani kwaiyo automatically ni watu wa kuwaheshimu na hiyo ni nguvu ambayo Mwenyezi Mungu kaiweka kwaiyo huwezi ukarekodi vitu kama vile alafu ukaviweka Kwenye mitandao inakuwa inaleta picha mbaya kama vile dada zetu hawana thamani kitu ambacho sio cha kweli”.

Tangu kitendo hiko kitokee siku chache zilizopita tayari Diamond ameshachukuliwa hatua za kisheria na Waziri amehaidi atafikishwa mahakamani kwa kitendo hiko alichofanya.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.