Nuh Mziwanda aomba mashabiki wake ushauri kuhusu wanawake

Nuh Mziwanda hajafanikiwa kuwa kwenye uhusiano unaodumu; baada ya kuwachana na muimbaji Shilole staa huyo alimuoa kipusa Nawal ambaye alimzalia mtoto wa kike.

Nawal na Nuh hata hivyo walikorofishana kwa ndoa yao kwa kiwango kuwa walifikia maamuzi ya kuwachana na kila mmoja kuenda zake.

download latest music    
Nawal na Nuh

Nuh sasa ameshindwa namna ya kupata mwanamke ambaye atadumu kwenye uhusiono na yeye. Staa huyo hatimaye aliamua kuomba ushauri kwa mashabiki wake jinsi ya kupata mwanamke atakayemfaa katika maisha yake.

Nuh na mwanawe

“Nimejifunza mengi sana kwenye life style yangu ya kimapenzi na najitoaga sana ila siku ya mwisho naumizwa ‘je unahisi Mwanamke wa aina gani atanifaa na nitaweza kudumu nae?Leo Nawaachieni mashabiki wangu mmalize hili ? #BaoLaUshindi,” Nuh Mziwanda aliandika kwenye mtandao wa Instagram.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere