Nuh Mziwanda azionyesha picha za mwanawe na mke wake

Image: Nuh Mziwanda

Wasanii wengi sasa hivi wameamua kuanza familia zao kwani hawana muda wa kungojea tena. Mmoja wao ni Nuh Mziwanda ambaye alibarikiwa na mtoto wa kike hivi karibuni na kama wasanii wengine ameweka picha ya mwanawake akiwa na mke wake.

Msanii huyu aliposti picha hizi katika mtandao wake wa Instagram akiziweka fikra zake wazi kupitia ujumbe aliomuandikia mtoto wake Anya na mamake. Mtindo huu pia tumeona na Diamond Platnumz na pia Rayvanny ambaye alibarikiwa na mtoto wa kiume hivi karibuni.

download latest music    

Nuh Mziwanda aliandika kusema…

Mungu pekee anajua jinsi gani moyo wangu na mihangaiko yangu inakulenga wewe Mwanangu #ANYAGHILE nasali sana Mungu akupe hekima ,busara ,upendo ,heshima kwa kila rika na upeo wa kujua baya na zuri ‘Nakupenda Mwanangu ANYA nipo kwa ajili yako kipenzi changu haijalishi nitaenda magharibi wala kusini katika hii dunia ? @iam_mrs_mziwanda #anameremeta video link on my bio @89studios #MariaStopesMwenge #DkSele

Tazama picha hizi hapa chini.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua