Nuh Mziwanda Bado Anateswa na Penzi la Shiloleh

Msanii wa muziki wa Bongo fleva, Nuhu Mziwanda amefunguka kuwa aliyekuwa mpenzi wake wa zamani, Shilole ni mwanamke pekee aliyemfundisha maisha na majukumu akiwa kama mtoto wa kiume.

Nuh amefunguka hayo kupitia DADAZ ya East Africa Television, ambapo amesema kuwa mwanadada huyo ndiye aliyekuwa mpenzi wake wa kwanza aliyemzidi  umri na tayari alikuta akiwa mwenye familia.

download latest music    

Shilole ndio mwanamke wangu wa kwanza aliyekuwa kanizidi umri, na amenifundisha majukumu na maisha pia baba anatakiwa kuwa vipi ndio chanzo cha mimi kuchora ‘tatoo’ ya jina lake mkononi kwangu hata tulipoachana sikuwahi kuifuta kwakuwa itabaki kuwa sehemu ya maisha yangu”, amesema Nuh.
Nuh na Shilole waliachana na baada ya muda msanii huyo alifanikiwa kufunga ndoa na mwanadada Nawal aliyefanikiwa kupata nae mtoto mmoja na baadaye waliachana pia.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.