Nuh Mziwanda ni Mwanaume Asiyejua Kutunza Siri

Msanii wa Bongo fleva Nuh Mziwanda amenyooshewa kidole na baadhi ya watu kwa tabia yake Kupenda kuimba kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi na kuyaanika hadharani.

Nuh ni moja kati ya wale wasanii ambao wanapenda kuimba kuhusiana na uhalisia wa maisha yao lakini kwa upande wa Nuh yeye anapendelea kuimba kuhusiana na mahusiano yake ya kimapenzi hasa na wapenzi ambao ameshaachana nao.

download latest music    

Hili lilionekana na yeye alivyotoa wimbo wake wa ‘Jike shupa’ ambao alimuimbia aliyekuwa mpenzi wake Shilole baada ya kuachana ambapo kwenye wimbo huo alimtafuta video queen ambaye alikuwa anafanana na Shilole na kuonyesha baadhi ya mambo yaliyokuwa yanatokea kwenye Mahusiano yao kama vile Shilole kumpiga Nuh na kurudi nyumbani usiku akiwa amelewa sana.

Lakini pia hilo limeoneka tena kwenye video yake mpya ya wimbo wake wa Upofu ambapo inasemekana kamuimbia aliyekuwa mke wake Nawal ambaye lakini pia amezaa na urban mtoto mmoja anayeitwa Anya ambapo kwenye video hiyo pia ametafuta video queen anayefanana na Nawal.

Baada ya tuhuma hizo Nuh Mziwanda alifunguka haya alipofanya mahojiano na Enews ya East Africa Tv:

Napenda kuwa huru napenda kufanya vitu vyangu ili watu wajue kile kilishatokea kilishapita kulikoni unatembea mtu anaona una kitu moyoni kwaiyo inabidi ukubali matatizo yako ili uweze kuyamaliza yaishe ili uweze kuendelea kwaiyo siku zote mimi ni mkeweli siwezi kuficha kitu  mimi hata nikimsaliti mwanamke wangu nitamwambia ukweli siwezi kukaa na kitu moyoni mpaka washakaji zangu wanapenda kuniambia mimi mmbea”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.