Ommy Dimpoz aeleza sababu zake za kukaa kimya kwa muda mrefu

Image: Ommy-Dimpo

Mkali wa nyimbo za bongo Ommy Dimpoz amekaa miezi kadhaa bila kuachilia project mpya. Japo anasemekana kuwa amepotezwa na vijana wadogo ambao wamekuwa wakionekana wamevalia sare zake na viatu muimbaji huyu ametoa stori nyingine.

Akizungumza katika interview Ommy Dimpoz alifunguka kwa kusema kuwa anauchukua muda wake kutengeneza kitu ambacho akiachilia mashabiki wake watafurahia.

download latest music    
Ommy Dimpoz

Aliendelea kwa kuongeza kuwa hajapotezwa na mtu yeyote kama watu wanavyosema. Alihaidi kuwa hivi karibuni ataachilia nyimbo mpya miezi kadhaa baada ya kufanya kazi na Alikiba.

“Siyo kweli kuwa nimepotea, kwanza najiandaa kuachia kazi mpya ambayo ina ubora wa hali ya juu, wanaosema nimepotea wasubiri waone maajabu yangu,”

Hata hivyo, Ommy Dimpoz ameonekana kunyamaza wakati ambao wasanii wa bongo wanapepea na nyimbo mpya.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua