Ommy Dimpoz Awatolea Uvivu Wasanii Wanaotoa Nyimbo Mbaya

Mwanamuziki wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amewatolea uvivu wasanii wenzake na kusema wanatoa nyimbo mbaya na wasanii wengine wanaogopa kuwachana.

Ommy Dimpoz amefunguka hayo Kwenye mahojiano na Magic Fm ambapo amedai wasanii wengi wanatoa nyimbo mbaya na hawajui:

download latest music    

Kuna nyimbo za wasanii wenzangu na nyingine unaona huu wimbo gani na unaona mwana anakomaa na ma-Interview”.

Lakini Pia Ommy Dimpoz amedai saa nyingine inakuwa ni vigumu kumtobolea na kumwambia mshkaji wako kuwa nyimbo ni mbaya kwa sababu anakuwa ameshawekeza.

Na siku zote wasema ukweli wanachukiwa, kuna siku niko na washikaji jamaa anamwambia mwana lakini ule wimbo wenu mnaenda ku-shoot video?, mbona ngoma mbaya, nikasema unatoa wapi ujasiri wa kumwambia mtu hivyo”.

Hivi sasa Ommy anafanya vyema kabisa na ngoma yake ya Yanje aliyomshirikisha msanii Seyi shay kutoka Nigeria.

Nyimbo hiyo imekuwa ikishika chati za juu tangu ilipotoka wiki iliyopita Kwenye mtandao wa Youtube.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.