Paschal Cassian Amshukuru RC Makonda Kufanikisha Safari Yake Ya India

Mshindi wa shindano la Bongo star  search (BSS) mwaka 2009 Paschal Cassian ambaye yupo hoi hospitalini Muhimbili kutokana na ugonjwa wa miguu amepata pesa ya kwenda India Kwa ajili ya matibabu.

Siku ya jana Msanii Mrisho Mpoto ametibitisha kuwa tayari mipango yote ya kwenda kumtibu Pascal Cassian nchini India imekamilika licha ya kwamba Pascal amejikuta akipata changamoto ya Passport ya kusafiria.

download latest music    

Katika mahojiano aliyofanya na Millard Ayo, Paschal Cassian amemshukuru RC Makonda kwa mchango Wake katika kufanikisha safari yake ya kwenda India.

Namshukuru mkuu wa Mkoa Makonda kwa kulibeba hili jambo kama la mtoto wake wa damu lakini changamoto niliyonayo kwa sasa sina Passport mimi na mke wangu, nina omba kwa RC Makonda na Rais Magufuli najua anaona so naomba sana kwa hii serikali pendwa inayosaidia wasiojiweza wanisaidie mimi na mke wangu kusudi niweze kusafirishwa”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.