PCK Aweka Wazi Mipango Ya Ndoa na Wema

Mpenzi wa staa wa Bongo movie Wema Sepetu anayejulikana kama Patrick Christopher maarufu kama PCK ameibuka na kutangaza ndoa na Wema Sepetu.

Global Publishers wanaripoti kuwa Mahaba ni mazito kati ya Wema na PCK na kuwa Mrembo huyo atakuwa nchini Burundi kwa muda wa mwezi Mzima sasa kwa ajili ya kutambulishwa kwa ndugu wa PCK wanaoishi huko.

download latest music    

Lakini pia inaripotiwa kuwa Wema amekolea vibaya mno kwa mwanume huyo kiasi ya kwamba humaambii kitu lakini inadaiwa Familia ya Wema haimtaki PCK kutokana na taarifa za utapeli zinazosambaa Kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko, PCK ameweka wazi kuwa ameshajitambulisha nyumbani kwa Wema na ndoa yao inatarajiwa kufungwa hivi karibuni mara tu watakapotejea Kwenye Safari yao ya Brazil walipo hivi sasa.

PCK amekiri kuwa atamuoa Wema Mke wa Pili kwani dini yake ya Kiislamu inaruhusu na kukiri  tayari ana Mke mmoja.

Lakini pia PCK amekana taarifa za yeye kuchukiwa na Familia ya Wema na kudai sio za kweli na kakataa tetesi za utapeli na hata taarifa za kufikishwa polisi baada ya yeye na Wema kutapeli watu.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.