Pedeshee Lammwaga Lulu Diva.

Mwanadada Lulu Diva amejikuta katika wakati mgumu baada ya Kuzagaa kwa  tetesi kuwa yule mwanaume ambae hapo awali aliwahi kuripotiwa kumpa kila kitu cha ndani na kumkabidhi mkoko ameamua kufunga  virago vyake na kuondoka na kumuacha mwanamke huyo solemba.

Watu wa karibu wa Lulu Diva wanasema kuwa mwanadada huyo amekuwa akifanya mambo hayo kwa siri kwa sababu hataki watu wajue hasa kwa sababu  mwanadada huyo amenyanganywa baadhi ya vitu vingi vya thamani ambavyo alinunuliwa ikiwemo gari.

download latest music    

Hata baada ya GPL kupata ubuyu huo waliamua kumtafuta Lulu diva kokote na ndipo walipomkuta nyumbani kwake hapo Mbezi Beach ambapo baada ya kuulizwa Lulu Diva alisema kuwa yeye ni mwanamke na ameamua kujiongeza kuachana na mwanaume huyo kutokana na kuwa hakuwa mwaminifu kwake  na kukanusha kuwa sio kuwa ameachwa bali wameachana.

Hata hivyo diva anasema kuwa hajanyanganywa nyumba wala gari kwa sababu ana uwezo wa kulipa kodi nyumba hiyo na kuhusu gari halijachukuliwa bado analo.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.