Penzi La Amber Lulu Na Prezzo Sasa Ni Mubashara.

Mwanadada Amber Lulu ambae mara ya kwanza alikanusha kabisa kuwepo kwa mahusiano katika yake na msanii kutoka Kenya Prezzo  baada ya kusamba kwa baadhi ya picha zilizokuwa zikiwaonyesha wako pamoja huku ikisema kuwa Prezzo alitoka Kenya kuja mpaka Tanzania kwa ajili ya kulifata penzi la mwanadada huyo. Wawili hao hivi sasa wameshindwa kuendelea kuficha tena  mahusiano yao kutokana na picha nyingi zinazoendelea kusambaa katika mitandao wakiwa pamoja sehemu mbalimbali huku msanii Prezzo akiwa ametoa wimbo ulikuwa na maneno ya kumsifia mwanadada huyo.

Hata hivyo mwanadada huo mbae amekuwa akimwagiwa sifa kemkem kutoka kwa mwanaume huyo ameonekana kufurahi na kulewa sifa hizo katika mitandao ya kijamii.Akielezea jinsi anavyojisikia kutokana na sifa anazomwagiwa tena hasa katika wimbo  mpya ambao Prezzo ameuachia huku akisema kuwa anampenda sana amber lulu,ni mzuri na ana roho nzuri na ameshamtambulisha kwa mama yake Amber Lulu anasema kuwa kwake ni furaha kuimbwa na msanii huyo na anajiona kuwa ni msichana mzuri kukubalika na watu wa nje.

download latest music    

Najisikia vizuri sana kusifiwa na prezzo,  maana mtu ukikubalika mbele ya mtu fulani  lazima ufurahi kwa kweli , ni mtu wangu wa karibu na tuna mpango wa kufanya kazi pamoja.Na kuhusu uchumba na kutambulishana  kwa mama yake ilo ni swala la siri kidogo kwa sasa kati yangu na yeye ,ikifika muda muafaka basi tutawaambia-amesema amber Lulu

Amber Lulu ambae alianza kupata umaarufu wake kupitia kuonekana katika video za wasanii mbalimbali nchini  alijitahidi na kufanya jitahada zake na kuanza kufanya vizuri na kuingia katika kuimba ambako pia alikuwa na anaendelea kufanya vizuri pia.

Ingawa amepitia mahusiano mengi nyuma na watu maarufu tofauti tofautri,mwanadada huyo ambae sasa hivi ameona bora kujiweka kwa msanii kutoka kenya anaonekana kufurahishwa na penzi ilo.Amber Lulu pia ni rafiki wa karibu wa msanii wa bongo fleva Gigy Money ambae walianza kustrugle na maisha wakiwa wote na mpaka sasa hivi wako wote kama marafiki.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.