Penzi la Aunty Ezekiel na Mose Iyobo Ladaiwa Kuwa Matatani

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Aunty Ezekiel amesemekana kuwa matatizoni na mpenzi wake Moses Iyobo ambaye ni mcheza shoo/ dancer wa Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Aunty Ezekiel na Mose Iyobo wamezaa pamoja mtoto mmoja wa like anayeitwa Cookie, mwanzoni wakati mahusiano yao yanaanza wapo watu wengi sana ambao waliponda kwa kudai kuwa Aunty hana hadhi ya kuwa na mtu kama Iyobo ambaye ni mcheza shoo lakini wenyewe walipendana na walilidhihirisha hilo. 

download latest music    

Aunty na Iyobo ni moja kati ya couple chache Bongo za mastaa ambazo hawana sana skendo mtandaoni au hawana sana kiki lakini kuna mara chache ambazo Aunty alitumia mitandao ya kijamii kulalama kuhusiana na uhusiano wake na Iyobo.

Miezi michache iliyopita Aunty Ezekiel alitumia ukurasa wake wa Instagram kumlalamikia mwanamke amnaye alikuwa anajigonga kwa Mose Iyobo na alifunguka nakudai kuwa mwanamke huyo alikuwa amedhamiria kumharibia familia yake.

Tangu hapo kumekuwa na tetesi kuwa penzi la Aunty na Iyobo limekuwa likilega lega ingawa hakuna hata mmoj kati yao aliyethibitisha tuhuma hizo.

Siku ya Jana Aunty aliandika maneno yaliyowapelekea watu wengi kudhani kuwa labda ni kweli penzi lake na baba watoto wake Moses Iyobo liko matatani. Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka picha inayomuonesha akiwa na mawazo makali alafu akaisindikiza kwa maneno yafuatayo:

Sina kawaida ya kuweka maisha yangu kwenye mitandao ya kijamii ila huku tunakoenda dah! Wanaume?”.

Maneno hayo ndio yalizidi kuzua tetesi kuwa labda penzi la Aunty na Iyobo limekufa kwa maana ni juzi tu Iyobo aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa anatamani kungekuwa sehemu ya wakina baba kudai haki zao wakinyimwa unyumba maana amenyimwa unyumba na Aunty!.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.