Penzi La Jacky Na Brown Matatani Tena

Msanii wa Bongo Movie Jackline Wolper na mpenzi wake Brown wamejikuta wakiaanza kuongelewa tena katika mitandao kuhusu mahusiano yao ambayo yana dalili za kuonekana kuvunjika, wawili hao ambao walikuwa wakiandamwa kwa muda mrefu katika mitandao huku baadhi ya mashabiki wakimtukana Jacky kuhusu umri mdogo wa mwanaume aliyenae.Hata hivyo kwa muda sasa Jacky amekuwa akimkingia kifua mpenzi wake huyo na kujibu tuhuma zote zinazomuhusu ikiwa hata kutukana mashabiki zake ilimradi tu kumuweka mpenzi wake huyo katika hali ya usalama.

Wikiendi iliyopita kulikuwa na shamrashamra nyingi kutokana na mfululizo wa sherehe za msanii mkubwa Diamond Platinumz kutimiza kadhaa, sherehe ambazo zilihudhuliwa na baadhi ya watu maarufu nchini.Hata hivyo katika kilele cha sherehe hizo zilizzofanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency Jackline Wolper alikuwa ni mmoja wa wasanii walioalikwa katika party hiyo ,lakini swali  ni kwanini Jacky hakutokea katika shughuli iyo na mpenzi wake huyo mpya.

download latest music    

Hata hivyo kuna picha zilizosambaaa mitandaoni , zinazomuonyesha msanii huyo wa kike wakisalimiana kwa kupeana mikono na mpenzi wake  wa zamani Harmonizee, inasemekana kuwa baada ya picha hizo kusambaa mpenzi mpya wa Jacky(Brown) alifuta picha zote za Jacky katika kurasa zake  za instagram.Swali linakuja je, kuna nini kinaendelea kati ya wawili hao, je ni kweli wameachana kutokana na wivu wa picha ya Jacky na Harmonize?Au ugomvi wao ulikuwa kabla ya hapo?

Akijibu tuhuma hizo, kupitia U Head ya XXL  ya Clouds Tv, Jackiline Wolper alipoulizwa kuhusu kufutwa kwa picha zake katika instagram ya mpenzi wake alijibu kuwa yeye hajui chochote taarifa hizo ndo anazipata muda huo,'”Kumbe kafuta, mimi sijaingia instagram,mi sijaona soudy huwezi ukaamini, izo taarifa ndio unanipa wewe” aliongea Jacky katika simu

Hata hivyo Jacky alipoulizwa sababu za mpenzi wake huyo kutokuudhulia katika party hiyo alisema kuwa , mpenzi wake huyo sio mtu wa kuudhuria katika party , huwa hapendi sana na mpenzi wake huyo ni siku ya tano sasa anaumwa kichwa pamoja na malaria , na hata hivyo yeye kutokea katika ile party ni kwa sababu ya heshima ya Diamond na sio vinginevyo.

kuhusu kufuta picha Jacky alisema kama amefuta ni kwa sababu maneno ya watu wamemfanya mpenzi wake huyo kupanick tu, lakini hawana ugomvi wowote.Lakini hata hivyo mpaka sasa Jackline Wolper amefuta picha zote za bff wake huyo na bff nae amemuacha kumfuata Jacky katika ukurasa wa instagram (unfollow)

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.