Penzi la Tunda na Diamond Lazidi Kufichuka, Tunda Kuonekana Madale.

Hakuna  penzi la siri hata  siku moja na hata kama mtajitahiid kulificha vipi ipo siku itajulikana hasakama mtaamua kuendlea na penzi hilo.Inawezekana Diamond anashindwa kujifunza kutokana na mambo kadhaa yanayomtokea kwa wanawake anaotembea nao lakini pia wapo mashabiki ambao kutwa kucha wanakuwa macho kwa ajili ya kuangalia nani kafanya nini na kuwa na muda wa ku-prove kama kitu fulani kinatokea au la.

Imepita muda kidogo tangu kuwepo na skendo za hapa na pale kuhusu penzi kati ya Tunda na msanii mkubwa Diamond Platinumz, ambapo inavyosemekana ni kuwa wili hao kwa sasa wana mahusiano ya kimapenzi tena hasa baada ya kuwa wanonekana baadhi ya sehemu pamoja ingawa wanafanya kwa siri.

download latest music    

Lakini pia kumekuwa na vita kali kati ya Tunda na Hamisa, mwanamke ambae amezaa na Diamond mtoto mmoja wa kike, Tunda amekuwa akirusha madongo gizani huku yakilenga kumpata Hamisa ambe pia alishapitia majanga mengi ya kugombana na mzazi mwenzie na Diamond (Zari) kwa sababu hiyo hiyo.

huko mitandaoni mashabiki wameanza kumpa taarifa zari juu ya uwepo wa tunda kila siku madale ambako diamond anaishi na kuna baadhi ya picha zikimuonyesha hata mdogo wake wa kike na mwandada tunda akiwa hukohuko madale ambapo famili hiyo kwa sasa wameweka kambi.

moja ya mashabiki alimwambia zari kuwa kwa sasa tunda anapika na kupakua  madale na zari alimjibu vibaya lakini swala ni kuwa taarifa hizi wanazokuwa wanampa Zari zinakuwa na ukweli ndani yake ingawa mwanamama huyo anaonekana kutojali na baadae yanakuja kutokea kama yaliyokuwa yanatokea kwa Hamisa.

                                                  

Alichojibu zari baada ya kuambiwa habari za Tunda.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.