Picha: Wachezaji wa Everton watangamana na wanafunzi Dar es Salaam

Klabu ya Everton kutoka Uingereza iliwasili Tanzania mapema leo kwa ajili ya kumenyana na Gor Mahia katika mashindano ya kombe la Super Cup linaloandaliwa na SportPesa ambayo ni mdhamini wa timu hizo mbili.

Wachezaji wa Everton leo wametembelea shule ya msingi ya Uhuru Mchanganyiko iliyopo jijini Dar es salaam na kushiriki michezo tofauti tofauti na watoto wenye ulemavu wa usikivu na uoni  hafifu.

download latest music    

Moja ya michezo walizocheza ilikua kandanda, wachezaji hao walifunikwa nyuso walipocheza na watoto wenye ulemavu.

Tazama picha hapo chini:

 

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua