Picha Za Brown Wa Wolper Akiwa Na Mwanamke Mwingine Zavuja

Imekuwa kama mtindo sasa kwa baadhi ya wasanii nchini na watu maarufu kuvujisha picha za utupa au wakiwa faragha na wapenzi wao.Picha zimevuja katika mtandao wa kijamii wa Instagam zikionyesha mwanaume ambae yupo katika mahusiano na msanii wa bongo movies na mjasiriamali maarufu Wolper  Jackline anaejulikana kama Brown zikimuonyesha akiwa na mpenzi mwingine tofauti na Jackline.

Picha hizo zimeleta gumzo kwa sababu wawili hao wanaonekana wapo faragha ilhali mashabki wa Wolper na mwanamitino huyo wanajua kuwa brown ana mahusiano na jackline na sio mtu mwingine yoyote.

download latest music    

Hata hivy wawili hao kuna kipindi cha nyuma ilisemekana kuwa walikuwa wamegombana kutokana na wawili hao kutokupostiana katika mitandao ya kijamii lakini walikuja wakakanusha na kusema kuwa hawajaachana, sasa swali linakuja kuwa je picha hizi zinaweza kuwa ni uthibitisho kuwa sasa hawapo pamoja tena?

Wolper akiwa na mpenzi wake Brown

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa wasanii wa bongo kuwa wanaachia picha chafu katika mitandao ya kijamii bila kujali ni nani anaangalia picha hizo.Hata hivyo hakuna aliyefunguka  kitu chochote tangu picha hizo kuvuja katika mitandao ingawa mashabiki wao wanaonekana kukerwa na tabia hizo.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.