Picha Za Chemical na Maxmizer Zaleta Utata.

Kwa muda mrefu msanii wa hip-hop nchini Chemical, amekuwa akijitapa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari  kuwa yeye ni single na hana mpango wa kujiingiza katika mahusiano hivi karibuni,huku akisema kuwa tangu utoto wake hakuwahi kujiingiza katika maswala ya mapenzi na hii ni kutokana na malezi mazuri aliyokulia kutoka nyumbani kwao.

Ilishawahi pia kusikika kuwa mwanandada huyo aliwahi kutamka kuwa yeye ni bikra(hajawahi kushiriki tendo la ndoa) na hii inawezekana iliwavutia wanaume wengi kwa sababu baada ya hapo watu wengi walikuwa wakisikia wakituma maombi kwake na hata yeye alikiri kuwa amekuwa akisumbuliwa sana na wanaume.

download latest music    

Lakini hivi karibuni mwanadada Chemical na Maxmizer walipiga picha na kusambaa katika mitandao ya kijamiiwakionekana wakiwa katika hali flani ya kimahaba, ambapo picha hzio zilizua utata na kuwafanya watu waamini kuwa sasa hivi Chemical ameamua kuachia baada ya kukaza kwa  muda mrefu na kuamua kujiingiza katika mahusiano.

Msanii mwenzie Stereo aliwahi kusikika katikia baadhi ya mahojiano akimuomba kumuoa Chemical lakini alikataa  na kusema kuwa kwa muda ule hakutaka kuwa katika mahusiano, lakini kwa picha zilizoanza kusambaa hivi karibuni zikimuonyesha wana-kiss na Maxmizer zinathibitihsa kuwa mwanadada huyo yuko tayari kwa sasa na amepata yule anaehisi ndie anaemfaa.

Chemical ni moja ya wasanii wa kike chipukizi wanaofanya vizuri katika muziki wa hip-hop , huku mara nyingi akiwa anajiwka katika muonekano wa kiume.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.