Picha Zilizovuja Zikimuonyesha Wema Sepetu na Mume Wa Mtu Zazua Gumzo

Muigizaji na mlimbwende Wema Sepetu, amejikuta katika wakati mgumu tena Jana usiku baada ya picha za faragha na bwana ake kuvuja mtandaoni.

Picha hizo zilizovuja zimewaonyesha wakiwa bafuni kwenye mahaba mazito. Inasemekana jina la mwanaume huyo ni Bakari Kila na kwa habari za chini ya kapeti zinadai kuwa mwanaume huyo ameoa na ana familia.

download latest music    

Picha za Wema na Bakari

 

 

Kupitia chanzo cha Global Tv inasemekana kuwa aliyevujisha picha hizi ni mtu wa karibu wa Wema kwani inavyoonekana hapo Wema ndiye alikuwa anapiga picha hizo. Mtu huyo aliyevujisha alisikika akiongea:

Achana na skendo ya unga inayomtafuna bwana wa Wema sahau kabisa zile picha zilizovuja Wema akiwa na Bakari mimi ninazo picha mpya wakiwa bafuni full mahaba, Wema ndani ya kanga moja huku wakipigana mabusu moto moto”.

Habari zilizopo zinadai kuwa kuna janga kubwa linaendelea baina yao, inasemekana kuwa bwana huyo wa Wema sio tu mume wa mtu bali pia ni muuza madawa ya kulevya na inavyosemekana kwa sasa yupo jela mjini Moombasa, Kenya.

Pia inasemekana kabla ya kutupiwa rumande bwana Bakari alikuwa na mkwanja mrefu sana ambao uliweza kumtuliza Wema mpaka akatulia na kuacha makeke ya mjini.

Pia picha hizo zimeonekana kuwakera sana mashabiki wa Wema hadi kuishia kumtolea mapovu makali.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.