Polepole Akutana na Wasanii Kuzungumzia Changamoto Zao.

katibu mwenezi wa chama  tawala nchini, Mh Humphrey Polepole amekutana na wasanii wa mzuki na miguzo nchini ikiwa ni kama mwakilishi wa serikali na kuongea nao mawili matatu yanayosumbua sanii nchini.

Wasanii wengi walijitokeza ikiwa ni kama wito wa serikali wa kutaka kukutana nao ili waweze kuzungumzia maswla yanayowahusu na kuona ni namna gani wanaweza kuayatatua ili kufanya sanaa ya tanzania iweze kuendelea mbele zaidi.

download latest music    

Ikumbukwe kuwa miezi michache nyuma  katibu mkuu wa chama icho alitangaza kuwa CCM haitawatumia wasanii tena katika shughuli za kichama hasa kampeni kwa uchaguzi utakao kuja kama ilivyokuwa kwa ule uliopita, jambo ambalo liliwafanya wasanii wengi kulalamika na hata kutuma salamu kwa Mh Rais kuangalia swala ilo.

Hata hivyo baada ya kikao icho kuisha hakuna kilichosemwa kuwa kimejadiliwa cha zaidi ya changamoto zinazokabili sanaa ya Tanzania , hivyo bado hakuna mrejesho wa swala hilo mpaka sasa.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.