Poshy Queen Ajibu Tuhuma Za Kutumia Mchina Kutengeneza Shepu

Socialite maarufu kwenye Mitandao ya kijamii Jackline Obeid maarufu kama Poshy Queen amefunguka na kuvunja ukimya Baada ya shepu yake kutengeneza headlines.

Kuna tetesi zilisambaa kuwa Poshy Queen ametengeneza umbo nchini Afrika Kusini na kuwa na muonekano tofauti na alivyokuwa zamani, mwenyewe ametoboa kuwa ameamua kunyamaza kwa kuwa hakuna anayemlisha.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Poshy alisema kuwa aliamua kunyamaza kwa sababu ameshangazwa sana na watu ambao wanavumisha hiyo skendo ya yeye kutengeneza shepu.

Unajua nilinyamaza kwa sababu niliona wazi sina cha kuwaambia kabisa maana wao ndio wamekuwa wakinijua zaidi kuliko hata familia yangu. Kwanza picha wanazozisambaza ni za zamani wakati nikiwa mwembamba na si vinginevyo.

Halafu kingine katika hilo kuna mambo mengi ya wivu na kutaka kuchafuana utaona hata ile picha wameitengeza nionekane sina kitu kabisa lakini mimi nimeachana nao kwa sababu hakuna mtu hata mmoja anayenilisha au kujua maisha yangu”.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.