Pretty Kind na Calisah Wadaiwa Kuwa Kwenye Penzi Zito

Muigizaji wa Bongo movie na msanii wa Bongo fleva Suzan Michael amedaiwa kuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na Model maarufu Calisah Abdulhameed.

Calisah ambaye ameshakuwa Kwenye Mahusiano na mastaa kadhaa kama vile Jacqueline Wolper na Wema Sepetu amesemekana kuweka kambi kwa Pretty Kind.

download latest music    

Global Publishers wanaripoti kuwa chanzo ma­kini kilieleza kuwa Pretty Kind amekuwa akioneka­na mara kwa mara maeneo ya Sinza, Dar akiwa na Calisah wakionyeshana mahaba niue hivyo ndiye mtu wake kwa sasa.

Baada ya Tetesi hizo kusambaa hivi karibuni gazeti hilo lilimsaka Pretty Kind ili kujua ukweli wa mambo Lakini mara moja alikataa taarifa hizo na kudai Hazina ukweli wowote.

Siyo kweli tupo karibu na Calisah kwa sababu ya kazi na siku ikimalizika mashabiki wataiona”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.