Prezzo: Bado Nampenda Amber Lulu

Mwanamuziki kutoka 254 Kenya, Prezzo amezidi Kupitia penzi lake kwa aliyekuwa mpenzi wake msanii wa Bongo fleva na video vixen Amber Lulu na kudai kuwa bado anampenda.

Wiki chache zilizopita kwenye birthday party ya Amber Lulu aliweka wazi kuwa ameachana na aliyekuwa mpenzi wake Prezzo na kumtambulisha rasmi mpenzi wake mpya anayeitwa Sam.

download latest music    

Habari za wawili hao kuachana zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii hasa baada ya kuacha kupostiana Kwenye mtandao wa Instagram kama ilivyokuwa kawaida yao.

Prezzo alifanya Interview na FNL ya EATV ambapo yupo nchini Tanzania kwa ajili ya kutangaza rasmi nyimbo yake mpya aliyofanya na Dogo Janja inayoitwa ‘Hamsamia’.

Kwenye mahojiano hayo Prezo alikataa kukubali kama kweli wameachana bali alisisitiza kuwa bado anampenda Amber Lulu na alipoulizwa kwa nini hakumposti Kwenye birthday yake alifunguka:

Kwani unajua birthday ngapi mama yangu hajaniposti Kwenye Instagram na sio kama hanipendi ananipenda ila ndio hivyo sio lazima kumposti ndo watu wajue kama unampenda kwaiyo mimi sikumposti Amber Lulu lakini Bado Nampenda”.

Prezzo alipotakiwa kuongelea kuhusiana na Amber Lulu kumtambulisha mpenzi mpya na kusema ameachana naye alikataa kata kata na kukimbilia kubadilisha mada.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.