Professor Jay aongelea hatma ya Diamond Platnumz bungeni

Mbunge wa Mikumi Joseph Haule maarufu kama Professor Jay amefikisha hatma ya Diamond na wasanii wengine kataka Bunge la Tanzania.

Professor Jay alieleza bunge changamoto zinazowakumba wasanii aliposimama kuchangia mapendekezo yake katika bajeti ya Wizara ya Habari, utamaduni, sanaa na michezo kwenye bunge la Bajeti linaloendelea.

download latest music    

Alisema TRA na mamlaka zingine za serikali zinawanyanyasa wasanii kwa kuwatoza kodi na ada zingine ambazo wasanii hawazi kumudu.

“Juzi msanii Diamond alikua analalamika TRA wamempelekea kodi ya milioni mia nne, kwa hivyo unaweza ukajiuliza kwamba amekabiliwa milioni mia nne kwa kiasi gani alichoingiza. Lakini dangozi ambazo zinafanyika munaweza mukaona kwamba sasa hivi wasanii wanabanwa, TRA wanatamani kuvuna kutoka kwa wasanii kitu ambacho bado hawajakibandikiza,” Professor Jay aliambia bunge.

Tazama video hapo chini:

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere