Q-Chillah Aelezea Jinsi Alivyotaka Kujiua, Ametangaza Rasmi Kuacha Muziki.

mwanamuziki mkongwe wa bongo fleva amefunguka mengi alupokuwa akiongea na dizzim online  baada ya waandishi wa habari baada ya tetesi kusambaa kuwa msanii huyo ameamua kuacha muziki na kuamaua kufanya vitu vingine.

q chillah amefunguka na kuelezea wakati mgumu aliowah kuupitia kipindi cha nyumba hasa baada ya kujiingiza katika madaw aya kulevya mabapo ilimchukua muda mrefu mpaka kurudi katika game na kusema kuwa maamuazi makubwa ya kauachana na madawa yalikuja baada ya kuona kuwa kuna kuwa na hukumu kubwa sana kwa familia yake wanapokuatana na jamii inayowazunguka.

download latest music    

q-chillaha nasema kuwa alikuwa akihumia sana anaposikia watoto wakimuuliza maswali magumu sana ambayo walikuwa wakiyasikia wakiwa shule au mtaani na hiyo ndio ilimfanya kuomba msaada na kuamua kuacahana na vitu hivyo kabisa .

Hata hivyo q-chillah anasema kuwa kuna kipindi alitaka kujiua akiamini kuwa hiyo ndio njia sahihi ya yeye kupambana na matatizo yake lakini alipanza kusali na kuingia katika toba aliomba kuondolewa mawazo hayo huku mawazo yake mengi yalikuwa yakimpeleka kuokoka kwa sababu muda mwingi alikuwa akisikiliza nyimbo za dini kutokana na anguko la kiimanai alilokuwa nalo.

Q-Chillah anasema kuwa anafurahi kuona wasanii wengine wakifanikiwa na kwenda nje ya nchi wakarudi na tuzo na kuamini kuwa hicho ndicho kitu kikubwa mabacho walikuwa wakikitafuta kwa muda mrefu na kimefanikiwa lakini anaamua kuchukua maamuzi ya kuacha muziki huku akiamiani kuwa inawezekana muda wake wa kuendesha gurudumu hilo umekwisha na kuwapisha wengine kuendelea nalo.

Q-Chillah anasema kuwa alitaka kutoa wimbo wake wa mwisho lakini roho nyingine inamtaka kuacha kutoa nyimbo hio lakini kitu kikubwa anachoamini ni kwamba  ameamua kuacha muziki lakini anataka kuacha kwa kuaga kwa heshima maana asipofanya hivyo ni kama anaogopa .

Q-chillah anakubali kusema kuwa anacaha muziki lakini inauma sana yeye kuacha muziki na ndugu na watu wake wa karibu wengi hawakukubaliana nae na hata yeye mwenyewe hajui anakwenda kufanya nini lakini anatamani sana kuendelea ila anaona kuwa ni bora kuacha muziki.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.