Q-Chillah Atangaza Kuendelea Na Muziki Aweka Kando Mawazo Ya Kuacha

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva aliyewahi kutamba na kibao chake ‘Ulinikataa’ miaka ya nyuma Q Chillah ameweka pembeni mipango yake na ya kuacha muziki na kuendelea kupambana.

Wiki iliyopita Q Chillah aliwashtua watu wengi pale alipofanya Interview na kutangaza kuachana na muziki kwa kila alichodai kuwa amekuwa akifeli kwa kila wimbo anaotoa kwa hivi sasa.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Q Chillah amedai baada ya kupata ushauri wa watu wengi tangu atangaze kuachana na muziki ameamua kuendelea kupambana:

Kinachonitafuna mimi ni mimi mwenyewe, maisha yangu ya nyuma yananihukumu. Lakini I don’t want to be a prisoner of my past”

Tangu nimetangaza kuacha muziki, nimeona mapenzi ya watanzania, nimeona mahaba yao, mpaka nimejiuliza tatizo sio support ya watanzania, labda ni mimi, au sikupata msaada niliohitaji ili kufanikisha maendeleo ya kazi yangu”.

Wiki iliyopita Q Chillah aliweka wazi kutoakana na kuhangaaika na muziki alijikita akiingia Kwenye matumizi ya madawa ya kulevya yaliyosababisha mpaka kukimbiwa na mke wake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.