Q-Chillah: Sina Tatizo na Papi Kocha Wala Baba.

Msanii mkongwe wa bongo fleva nchini Q-Chief amefunguka na kusema kuwa hana ugomvi wala matatizo yoyote na wasanii Papii Kocha na baba yake lakini kuna baadhi ya watu wametaka kuwaonyesha umma kuwa wao ni maadui au kuna kitu wanataka kuwafanyaia ili waonekana kama hawapo sawa.

Maneno hayo ameyasema Q-Chillah siku chache baada ya kumalizika kwa show ya kuwakaribisha wasaii hao wawili Papii na baba yake Mzee Nguza baada ya kuwa nje ya game la muziki kwa muda mrefu kutokana na wao  kuwa gerezani.

download latest music    

Q-chillah anasema kuwa alipata ruhusa na barak zote kutoka kwa mc na hata wasanii wenye show yao lakini kitu cha ajabu alishangaa kuona mic inazimwa na akashindwa kuendelea na show yake kwa uda huo.

wakati mimi nina perfom wimbo wangu wa kwanza wa nikilala naota katika show yao nilipata baraka zote kutoka kwa mc na hata papii na baba pia,so kwenye kazi unapoona watu wana muitiko mzuri na wewe inabidi ujiongeze.na kutokana na mapezni yao na mimi ilibidi kufanya kazi yangu kama vile ninavyokuwa nafanya sehemu nyingine, kwa sababu natumia nguvu nyisa sana katika kazi zangu lakini kitu cha ajabu ile napanda tena jukwaani naona kipaza sauti kimezimwa.

Sitaki kuweka kuwa nilikuwa na tofauti nao lakini nilikuja kuzijua baada ya kuziangalia zile video vizuri baadae nilipokuwa na watuwangu wa karibu ndipo hata mke wangu aliponiuliza kimetokea nini.lengo langu lilikuwa ni kuroa burudani tu na kumfariji rafiki yangu ambae alikuwa nje ya ulimwengu wetu kwa muda mrefu, 

Hata hivyo Q-Chillah anasema kuwa kama kutokea kwa tatizo la kuzimwa kwa kipaza sauti basi ilo sio tatizo la Papii Kocha au baba ila lilikuwa ni tatizo la fundi mitambo aliyekuwepo kwa muda ule.

Sio tatioz la papi wala mzee wangu nguza kwa sababu wao waka hawaitaji stress sasa hivi,litakuwa ni kosa la wale waliokuwa wanashughilika na mitambo kule nyuma maana ndio anashugulika na vyombo vyote.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.