Queen Darleen Amwaga Povu Kuhusu Mavazi Yake Ya Ajabu

Mwanamuziki kutoka katika label ya WCB na Dada wa Staa wa Diamond Platnumz, Queen Darleen ameibuka na kuwamwagia Povu zito mashabiki ambao wamekuwa wakikosoa mavazi yake.

Queen Darleen amefunguka na kusema nguo anazovaa za kimitego zinazoacha sehemu kubwa ya mwili wake hazina madhara kwake na kwa mpen­zi wake.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Darleen Risasi Jumamosi kuwa, mara nyingi anaona watu wanamse­ma kuhusu nguo anazovaa, lakini hawajui kwamba yeye kama mwanamuz­iki ndizo nguo anazo­paswa kuvaa.

Kinach­onishangaza ukivaa kibukta, utasikia watu wanakusema umekaa uchi, sasa sijui wa­nataka nikiwa ninapanda stejini nivae khanga? Maana hata huyo mpenzi wangu haongei chochote kuhusu mavazi yangu jamani”.

Kwa muda mrefu sasa Queen Darleen amekuwa akikosolewa sana na mashabiki zake kutokana na mavazi yake ya kimtego ambayo amekuwa akivaa na kujianika kwenye mitandao ya kijamii.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.