Queen Darleen- Bado Nampenda Zari

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Queen Darleen ambaye pia amejipatia umaarufu kwa kuwa dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, amefunguka na kusema bado anampenda aliyekuwa wifi yake Zari.

Zari alimwaga aliyekuwa mpenzi wake Diamond Platnumz mwezi uliopita lakini mpaka leo bado wanatengeneza headlines kwenye mitandao ya kijamii kwa kuongelewa.

download latest music    

Queen Darleen amefunguka kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers ambapo aliulizwa kuhusu mawifi zake kwa Diamond hasa kwa sababu Amekuwa hatabiriki yupo upande gani maana bado ana urafiki na Penny ambaye alikuwa mpenzi wa zamani wa kaka yake.

Queen Darleen ameongelea mapenzi yake kwa Zari huku akikiri kuwa bado anampenda sana wifi yake huyo:

Kwanza kabisa watu wajue mimi nampenda sana Zari Tena sanaa lakini kiukweli huko nyuma nilimpenda Wema kwa sababu ndiye alikuwa ni wifi kwa kipindi hiko lakini Penny amebaki kuwa rafiki yangu hadi sasa”.

Lakini pia Queen Darleen alifunguka kuhusu Hamisa ambapo amedai yeye na Hamisa hawana mazoea sana anachojua yeye yule ni mama wa mtoto wao Abdul na walikuwa wanaonana kwenye masherehe tu huko nyuma.

Queen Darleen amekiri kuwa hapendi sana kumfuatilia Diamond na maisha yake binafsi kwani yeye hajawahi kumfuatilia hata siku moja.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.